Vyanzo vya maji moto ni njia mbadala wa kutengeneza nishati ya umeme

Habari hii ni kutoka NAIVASHA, KENYA, 27.4.2012

Wakati nchi iko katika mikakati ya kuanzisha vyanzo mbadala vya umeme kwa ajili ya kupata nishati ya kuchochea ukuuaji wa viwanda na kuboresha maisha ya wananchi, imebaika kuwa, vyanzo ya maji moto kama vile cha Mtagata katika kata ya Kamuli, vyaweza kuwa moja wapo ya kuzalisha umeme.

Maps showing the Olikario Geo-thermal plantHayo yamebainiwa na Mkrugenzi wa radio FADECO Joseph Sekiku, alipotembelea mradi wa kufufua umeme kutokana na mvuke utokanao na maji moto yanayobubujika kutoka ardhini ulioko katika wilaya ya Naivasha nchini kenya. Hapo jana, Bw. Sekiku ametembelea mradi huu ujulikanao kama OLIKARIA GEO-THERMAL PLANT ulioko nje kidogo ya mji wa Naivasha.

Mradi huu uliozinduliwa mwaka 2004 na rais Mwai Kibaki wa kenya, unao uwezo wa kuzalisha mega watts 105 za umeme kutokana na nguvu za mvuke kutoka ardhini. Mradi huu umeelezwa kuwa wa kwanza barani Afrika, na kuwepo kwa mradi huu, kumeweza kupunguza shida za umeme hasa kukatikakatika mara kwa mara na kutokuwa na umeme wa kuendesha shughuri za maendeleo.

Akizungumza na mtaalamu katika mradi huu, Bw. Kamau ambaye amekuwepo kuzungumza kuhusu mradi huu, amesema kuwa, hadi sasa, mradi huu umeweza kutoshereza mahitaji ya umeme kwa nchi wa kenya kwa asilimia 65% na kwamba, ifikapo mwaka 2015, Kenya itakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kujitoshereza na mwingine kuwauzia nchi jirani hasa Somalia na Ethiopia.kibao kinachoonyesha eneo la mradi wa geo-thermal, Olikario

Tekinolojia ya kufufua umeme kutokana na mvuke:

Joto kutoka ardhi, pia joto ardhi (Kiing.geothermal energy” kutoka Kigiriki geo =ardhi na thermos = joto) ni chanzo cha nishati kinachotumia joto lililopo katika ganda la dunia. Joto hili latokana na mchakato wa kinyuklia ndani ya tufe la dunia na kiasi kidogo kutoka joto la jua linalopokelewa kwenye uso wa dunia.

Tangu siku za kale watu walijua mahali kadhaa ambako maji ya moto yanatoka kwenye ardhi kama chemchemi. Kama chemchemi hizi za moto zilkuwa karibu na makazi ya watu zilitumiwa kwa kuogelea au hata kupasha moto nyumba kwenye mazigira baridi.

Lakini siku za nyuma watu waligundua mbinu kulitumia joto kutoka ardhi kwa kuzalisha umeme.[1] Mwaka 2007 takriban gigawati 10 za umeme zilipatikana kutokana na matumizi ya jotoa kutoka ardhini ambazo zilikuwa 0.3% ya mahitaji yote ya umeme duniani lakini katika nchi kadhaa kama Iceland au Kenya asilimia ilikuwa kubwa zaidi.

Katika mazingira ya volkeno joto kutoka ganda linafikia uso wa dunia na hapa ni rahisi kutumia mvuke unaotoka au akiba za maji moto zilizopo mita chache chin ya uso wa ardhi kuendesha rafadha za kutengeneza umeme. Nafasi hii iko pia katika sehemu za Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki ambako hadi sasa kuna vituo 3 vya joto ardhi katika Olkaria. [2].

Katika mazingira ya kawaida pasipo na volkeno au njia za magma zinazokaribia uso wa dunia kuna uwezekano kupeleka mabomba ardhini na kupitisha kiowevo kwa pampu katika mabomba haya chini ya ardhi. Tofauti ya joto kati ya kina ambako mabomba yanafikia na uso wa dunia hutumiwa kwa kupashaia nyumba joto au baridi.

Kama kiwango cha joto kinachotolewa ardhini hakizidi kiwango kinachozalishwa katika kina ya ardhi nishati inayopatikana hapa ni kama nishati mbadala.

MAPENDEKEZO KWA SERIKALI YA TANZANIA:

Kwa wakati huu serikali ya Tanzania inayo mikakati ya kuanzisha miradi ya kufufua umeme nchini ikiwemo kutumia nguvu za maji (HYDRO ELECTRICITY POWER GENERATION) katika mto Kagera na mito mingine nchini, kutumia mkaa ya mawe, kutumia gesi asilia (NATURAL GAS) na mikakati mingine mingi.

Kwa muda kaadha, Tanzania imekumbwa na uhaba mkubwa wa umeme kutokana na upungufu mkubwa wa maji katika mito na mabwawa ya kuweka maji ya kuzalisha umeme, na kupanda kwa gharama ya mafuta. Jambo hili limekwamisha maendeleo katika maeneo mengi na limeacha serikali ikiumia baada ya kulazimika kuanzisha miradi mingine mbadala ambayo imejifanya kutumia pesa nyingi na kubaki na madeni makubwa.

Kama ambavyo inakumbukwa, mgawo wa umeme umekuwa kitu cha kawaidia katika miji mikubwa huku uzalishaji ukishuka kwa asilimia kubwa. Awali, serikali iliingizwa katika matatizo baada ya kuingia katika makubaliano na makampuni kama vile ya Dowans katika kujaribu kutatua changamoto za uhaba wa umeme.

Hali ya umeme wilayani Karagwe:

Wilaya ya Karagwe ni miongoni mwa wilaya chache za nchi na mkoa wa Kagera
ambazo zinafaidika moja kwa moja na umeme unaotoka Uganda kupitia maporomoko
ya mto Nile. Hapa hakuna mgawo wala nini, umeme upo tu saa 24, ukiondoa siku
chache mno za services. Lakini ni wananchi wangapi wanatumia umeme? Umeme
umeingia Karagwe kwa kufuata njia kuu ya Kyaka tokea Bukoba hivyo
unapatikana tu kwenye maeneo ya njia kuu hii.

Sina takwimu sahihi lakini ninaamini umeme unapatikana kwenye maeneo ya njia
kuu ya Bukoba Karagwe hususani kwenye taasisi za serikali kama gereza la
Kitengule, Kikurura Ranchi, Kihanga, Kayanga yaliko makao makuu ya wilaya,
Omurushaka mji wa biashara na maeneo jirani na miji hii, basi! Hii ni kama
asilimia 1.5 ya wilaya ya karagwe.

Njia ya kuelekea Rwambaizi, umeme unaishia Ndama na katika njia ya kuelekea Nkwenda, umeme unaishia Ihanda. Njia ya kuelekea Bushangaro umeme unaishia kijiji cha Nyakahanga wakati njia ya kuelekea Nyaishozi kwa wakati huu pia umeme unaishia katika kijiji cha Nyakahanga.

Nimatumaini yangu kuwa mpango wa REA utawawezesha wakazi wengi wilayani karagwe kuonja utaamu wa umeme kwani tayari nguzo za umeme zimeisha tandazwa hadi Ihembe, ambapo matumaini kwa wakazi wa Bisheshe, Nyakayanja, Nyaishozi hadi Ihembe tayari wameanza kufanya wiring ya nyumba zao wakisubiri umeme kuwasili. Kwa wakazi wa maeneo mengine wilayani Karagwe, yawapasa kuwa na subira.

Mpango wa kufufua umeme mbadala kwa maeneo baadhi wilayani Karagwe:

Katika mto wa Kagera, upo mpango wa kufufua umeme katika eneo la Rusmo wilayani Ngara. Umeme huu utawezesha wananchi wa wilaya hususani ya Ngara, ambao hadi sasa umeme wao unatokana na genereta zinazotumia mafuta, kupata umeme wa kuaminika. Pia upo mpango wa kufufua mradi wa kutengeneza umeme wa Kikagati (karibu na Murongo) ambao unatarajia kuwanufaisha wakazi wa wilaya mpya ya Kyerwa.small hot water spring trapped for hot water domestic use

Na katika mantiki hii, eneo la mtagata katika kata ya kamuli, nalo laweza kujipatia umeme wa geo-thermal kutokana na chanzo cha maji moto katika eneo hilo.

About fadeco

Media expert from Tanzania.
This entry was posted in News from Karagwe - Tanzania, Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s