Wazazi wilayani Karagwe wahimizwa kuwapeleka watoto wao katika vyuo vya ufundi

17.11.2012 na Adelina Rweramula

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karagwe Mh.Kashunju Runyogote amewataka wazazi wa wilaya Karagwe kupeleka watoto shule pindi wanapo hitimu elimu yao ya msingi na sekondari.

Amesema hayo kwenye mahafali ya ishirini na nne (24) yaliyofanyika kwenye Chuo cha mafunzo ya ufundi wilaya Karagwe hapo tarehe 16/11/2012. Jumla ya wahitimu 88 wakiwa wasichana 26 na wavulana 62 wamemaliza masomo yao katika fani mbali mbali.

Aidha Mh.Kashunju Runyogote amesema kuwa chuo kilijengwa kwa ajili ya Wana Karagwe lakini inaonekana wanafunzi waliowengi wanatoka nje ya wilaya kama Misenyi na kwingineko kitu ambacho wazazi wa wilaya hii watajutia .

Hata hivyo Mh.Kashunju Runyogote amezidi kuwataka wazazi na walezi kutimiza ahadi zao kama baba na mama wanavyo wekeana ahadi kuwa wata saidiana kuwalea watoto watakao wapata wanapokuwa kwenye ndoa yao, hivyo moja ya ahadi ni hiyo ya kumpeleka mtoto shule na kumpatia matunzo muhimu

Sambamba na hayo Mh Kashnju Runyogote ameahadi kutoa shilingi Milioni mbili kwa ajili ya kununua mashine ya kusaga mahindi ikiwa ni moja ya njia ya kutatua changamoto zinazo kumba chuo hicho kama ilivyosomwa kwenye risala yawahitimu.

About fadeco

Media expert from Tanzania.
This entry was posted in HABARI ZA SIKU, News from Karagwe - Tanzania and tagged , , . Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s