Zaidi ya viongozi 70 kutoka katika mashirika na taasisi zinazowasaidia watu wenye ulemavu mkoani Kagera, wamehudhuria kongamano liloandaliwa na radio FADECO katika kilichoelezwa kama zoezi la kutoa taarifa ya utafiti juu ya watu wenye ulemavu wilayani Karagwe. Mkutano huo, umezinduliwa na mama Oliva Owibingire katika nafasi yake kama mjumbe wa bodi ya radio FADECO lakini pia akiwa mwenyekiti wa wanawake wilayani karagwe.
Watu wenye ulemavu ni moja wapo ya kundi la watu wasio na sauti kutokana na ukosefu walio nao wa viungo au hali anayokuwa nayo mtu wa kawaida. Changamoto wanazokumbana nazo ni nyingi ikiwa ni pamoja na unyanyapaji wakinyanyapaliwa na watu wengine lakini pia baadhi wao pia wakiwa wanajinyanyapa. Katika kongamano hili, takwimu zimeonyesha kuwepo kwa takribani watu 6,000 wilayani Karagwe wenye ulemavu, na wenye kuhitaji msaada ijapokuwa, hata uongozi wa halmashauri ya wilaya ulikuwa hauna taarifa zao sahihi wala kuwa na picha kamili ya changamoto walizo nazo.
Mafanikio yaliyotokana na mkutano huu
Mkutano huu uliweza kutoa picha na hali halisi ya watu wenye ulemavu ilivyo katika wilaya ya Karagwe na ripoti ya utafiti iliyotolewa na watalam wa radio FADECO, iliweza kuvuta hisia za watu waliohudhuria pale walipoona picha za watu wenye ulemavu.
Ni ukweli ulio wazi kuwa wadau,viongozi na wanajamii kwa ujumla waliohudhuria mkutano wa kuwasilisha ripoti ya utafiti juu ya watu wenye ulemavu wilaya ya Karagwe, waliguswa moja kwa moja na kushangaa idadi kubwa ya watu wenye ulemavu hapa wilayani. Pia na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka kila kata zipatazo 40 za wilaya hii, walijisikia faraja kwa namna walivyoshirikishwa na namna walivyohudumiwa katika kuwapa sauti watu wenye ulemavu.
Mkutano huu uliwapatia fursa viongozi wa kijamii na serikali kufikisha ujumbe wao haswa watu wenye ulemavu waliohudhuria waliweza kutambua vema ni kipi kinaendelea juu yao kuhusiana na hali halisi ya maisha yao.Kupitia utafiti huu na mkutano kwa ujumla wadau kadhaa waliweka ahadi mbele ya wadau pia mioyoni mwao kuwasaidia watu wenye ulemavu.
Hakika ili kuwa siku ya mwanga mpya kwa watu wenye ulemavu kukutana kwa pamoja na kujadili mambo yanayowagusa moja kwa moja wakiwa na jamii tofautitofauti maana walikuwepo wadau toka ndani na nje ya mkoa wa Kagera ambao walitoa mwamko mpya katika maisha ya watu wenye ulemavu na jamii kwa ujumla.
1.1 Mahudhurio
Namshukuru Mungu kuwa lengo lilitimia la kutoa taarifa ya hali halisi ya watu wenye ulemavu hapa Karagwe kwani viongozi wa kada mbalimbali waliweza kuhudhuria mkutano huu.Jumla ya wadau 85 walihudhuria mkutano huu ambapo viongozi wa madhehebu mbalimbali walihudhuriaviongozi wa kada mbalimbali wa kijamii na serikali pia nao walijumuika katika mkutano huu na kuleta maana halisi ya mkutano wadau.
Uwepo wa meneja msaidizi wa shirika la kuhudumia watu wenye nchini la CCBRT ambalo lina makao yake makuu Msasani jijini Dar es salaam ilikuwa ni mwanga mpya kwa watu wenye ulemavu ,kuwepo wa mwakilishi kutoka IZAAS MEDICAL CENTRE kutoka Bukoba,mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya wenye ulemavu mkoa wa KAGERA na katibu wake nao uliwapa fursa wadau kujua nini maana halisi ya ulemavu pia kujua lugha ambazo hazileti unyanyaapaa kwa watu wenye ulemavu hapa Karagwe.Mgeni rasmi ambaye alikuwa katibu Tawala wa wilaya ya Karagwe akimwakilisha mkuu wa wilaya COL Mstaafu Suleiman Issa Njiku,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe Kasunju Runyogote pia kulileta maana halisi ya mkutano wa wadau.
Vyombo vya habari navyo vilikuwa bega kwa bega kuhakikisha vinatoa sapoti muhimu katika kuhamasisha kwa undani zaidi ili jamii iweze kushiriki kikamilifu kupigania haki na maslahi ya watu wenye ulemavu zinatekelezeka..Wana habari walioweza kufika katika mkutano huu ni kutoka Sengerema FM-Mwanza, Kasibante Fm-Bukoba,Vision FM-Bukoba,Karagwe FM ,Fadeco Fm na waandishi wa Magazeti ,Blogs na taasisi ambzo zinashiriki kutoa elimu ya habari hapa nchini.Mwakili wa kutoka shirika la utangazaji la Uingereza BBC, Tony aliyezungumzia umuhimu wa vyombo vya habari katika kuisaidia jamii katika kufikia malengo yake kikamilifu.
Kuwa na idadi hiyo ya wageni ilileta na kuvuta hisia za wazi kwa watu waliohudhuria mkutano huu kiasi kwamba kuuliza mliwezaje kufanya kazi hii yenye kuhitaji uvumilivu.
Haya ndio maudhulio ambao waliweza kushiriki nasi katika uwasilishaji wa ripoti yetu ya utafiti.
1.2 GHARAMA ZA KUENDESHA MKUTANO.
Haikuwa kazi rahisi kuandaa na kuendesha mkutano huu maana ilihitaji gharama za mkutao huu.Mkutano huu ulikuwa umegawanyika katika makundi mengi tu kwani kuna watu wenye ulemavu kusafirishwa kulazwa ,kuhudumiwa kila aina ya huduma zote muhimu za kibinadamu.
Katika mkutano huu ambao ulirushwa moja kwa moja na redio Fadeco uliweza kuteka hisia za wanajamii na wasikilizaji wote ambao walikuwa wakifuatilia mkutano huu moja kwa moja kwa maana redio Fadeco inasikika wilaya zote za mkoa huu wa Kagera na maeneo jirani ya nchi ya Uganda.
Jamii ya wilaya ya Karagwe na mkoa wa Kagera kwa ujumla ilikuwa haijui baadhi ya aina za ulemavu lakini baada ya mkutano huu imeweza kubaini ni nini maana ya ulemavu na aina za ulemavu,pia kujua ni lugha ipi itumike ili kukomesha tabia ya unyanyapaaji wa watu wenye ulemavu. Lakini pia jamii imekuwa na uwezo wa kubaini watu wenye ulemavu kwa sasa na kwa asilimia nyingi wanajua nini faida ya kuwafichua watu wenye ulemavu maana mwanzo hawakujua umuhimu huo.
Watu wenye ulemavu waliokuwa na wao wakijinyanyapaa wameweza kufahamu wanalopaswa kulitenda hivi sasa hawajifichi tena maana kupitia idadi kubwa ya watu wenye tatizo la FISTULA wamejitokeza kwa wingi baada ya mkutano huu ambapo shirika la CCBRT kutangaza rasmi kuwa linasafirisha wenye tatizo la Fistula na mdomo wazi kuwa matibabu ni bure.
1.3 MCHANGO WA VIONGOZI WA DINI,SERIKALI NA TAASISI.
Kupitia mkutano huu wadau wa maendeleo ngazi mbalimbali waliweza kutoa ahadi zenye kuleta matumaini kwa watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kupunguza hali duni za watu wenye ulemavu ili waweze kukabiliana na changamoto walizonazo.
Mkurugenzi wa shirika la WOMEDA Juma Masisi ambaye ni mwanasheria kitaaluma aliweza kusema atashirikiana bega kwa bega ili kuwasaidia watu wenye ulemavu ktk utetezi wa haki zao.,Kanisa la KKKT kupitia idara ya Udiyakonia ambayo hushughulika na watu wenye mahitaji maalumu katika jamii kuhaidi kuwa itaweza kushirikiana kwa karibu na watu wenye ulemavu.Kanisa Katoliki jimbo la Kayanga kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya kujenga shule ya watoto wenye mahitaji maalumu katika eneo la Chabalisha ili kuwapa fursa ya kupata haki yaoya msingiya elimu.
Serikali kupitia kwa hotuba ya mgeni rasmi pia mwenyekiti wa halmashauri ndugu Kasunju Runyogote alibainisha hatua ambazo zimechukuliwa na halmashauri katika kuwahudumia watu wenye ulemavu ikiwa ni pomoja na kutenga sh 95 milion katika mwaka wa bajeti wa 2012/2013 kukamilisha ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu eneo la Chabalisha, kuwatengea sh million 5 kwa ajili ya kuendesha miradi midogo midogo kwa watu wenye ulemavu,imewapatia ofisi ambazo ziko katika jengo la Angaza Kayanga,sh milioni 2 zimetolewa kwa ajili ya kuendeleza karakana ya watu wenye ulemavu pia kuwasomesha walimu wa elimu maalumu ili waweze kufundisha katika shule hiyo.
2.0 MAFANIKIO YALIYOTOKANA NA MKUTANO HUU
Mafanikio ambayo yametokana na mkutano huu ni ya kujivunia hata kama si ya kujiridhisha kwa kiasi kilichokuwa kinahitajika lakini yafuatayo ni moja ya ishara ya mafanikio makubwa ya mkutano huu hii ni pamoja na
i)Jamii kutambua kuwepo na idadi kubwa ya watu wenye ulemavu na aina mbalimbali za ulemavu hapa Karagwe
ii) Kufahamu jukumu la viongozi ,wadau na jamii katika kuwahudumia watu wenye ulemavu katika wilaya ya Karagwe na mkoa kwa ujumla
iii)Viongozi ,wadau, na jamii kutoa tamko la kujifunga la kutekeleza jukumu la kuwahudumia wadu wenye ulemavu na makundi yenye mahitaji muhimu.
iv)Watu wenye ulemavu kupata fursa ya kukutana kwa pamoja kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo na jamii na kuionesha kuwa na wao wana uwezo stahiki ktk maendeleo kwa kutumia fursa zilizopo kwa ukamilifu.
V)Kuwepo mwanzo mpya wa matibabu kwa watu walikuwa wamekwisha kata tama ya kupona watu wenye matatizo ya ugonjwa wa FISTULA kuweza kupata matibabu bure.
vi)Kuondoa unyanyapaa miongoni mwa jamii lakini na kwa watu wenye ulemavu wenyewe maana walikuwa wanashindwa kujitokeza
vii)Kuondoa imani potofu ya kuamini kuwa ulemavu mwingine ni wa kurogwa au kuwa ulemavu ni laana lakini hiyo mitizamo imeweza kuanza kutoweka baada ya mkutano huo.
Viii) Kuwepo idadi kubwa ya wanawake wenye tatizo la Fistula kujitokeza kwa wingi kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa Kagera baada ya Radeo FADECO kurusha mkutano huu,Kwani mpaka sasa wagonjwa wapatao 16 wameisha safirishwa kwenda kutibiwa jijini Dar es salaam
ix) Serikali ya halmashauri kuamua kutenga bajeti kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha miradi midogo midogo
x)Kuwepo jitihada za kuunda vikundi kwa ajili ya kuwawezesha kuwa na vikundi imara.
Haya ni moja ya mafanikio ya mkutano huu lakini yapo mengi yaliyotokana na mkutano huu pia kuwepo na mwamusho mpya wa kuwa na mtandao wa watu wenye ulemavu.
2.1 HITIMISHO
Nahitimisha kwa kuwaasa wadau wote wa maendeleo wazawa tusisubilie misaada ya wahisani bali tunaweza kutatua matatizo yetu wenyewe bila ya kumtegemea mtu au wahisani ni jukumu moja linalohitajika ni kuwa na moyo wa kujituma na wa kizalendo zaidi katika kuwahudumiawatu wenye mahitaji maalumu.
KUMBE NIMEAMINI INAWEZEKANA KUWA NA MOYO WA KIZALENDO.
AHSANTENI