RADIO FADECO YAWAPA SAUTI WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KARAGWE

Zaidi ya viongozi 70 kutoka katika mashirika na taasisi zinazowasaidia watu wenye ulemavu mkoani Kagera, wamehudhuria kongamano liloandaliwa na radio FADECO katika kilichoelezwa kama zoezi la kutoa taarifa ya utafiti juu ya watu wenye ulemavu wilayani Karagwe. Mkutano huo, umezinduliwa na mama Oliva Owibingire katika nafasi yake kama mjumbe wa bodi ya radio FADECO lakini pia akiwa mwenyekiti wa wanawake wilayani karagwe.

Mr. Anthony from BBC MEDIA ACTION making his presentation in Role of Media in developmentWatu wenye ulemavu ni moja wapo ya kundi la watu wasio na sauti kutokana na ukosefu walio nao wa viungo au hali anayokuwa nayo mtu wa kawaida. Changamoto wanazokumbana nazo ni nyingi ikiwa ni pamoja na unyanyapaji wakinyanyapaliwa na watu wengine lakini pia baadhi wao pia wakiwa wanajinyanyapa. Katika kongamano hili, takwimu zimeonyesha kuwepo kwa takribani watu 6,000 wilayani Karagwe wenye ulemavu, na wenye kuhitaji msaada ijapokuwa, hata uongozi wa halmashauri ya wilaya ulikuwa hauna taarifa zao sahihi wala kuwa na picha kamili ya changamoto walizo nazo.

Mafanikio yaliyotokana na mkutano huu

Mkutano huu uliweza kutoa picha na hali halisi ya watu wenye ulemavu ilivyo katika wilaya ya Karagwe na ripoti ya utafiti iliyotolewa na watalam wa radio FADECO, iliweza kuvuta hisia za watu waliohudhuria pale walipoona picha za watu wenye ulemavu.

Chairman of SHIVYAWATA making his presentationNi ukweli ulio wazi kuwa wadau,viongozi na wanajamii kwa ujumla waliohudhuria mkutano wa kuwasilisha ripoti ya utafiti juu ya watu wenye ulemavu wilaya ya Karagwe, waliguswa  moja kwa moja na kushangaa idadi kubwa ya watu wenye ulemavu hapa wilayani. Pia na wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka kila kata zipatazo 40 za wilaya hii, walijisikia faraja kwa namna walivyoshirikishwa na namna walivyohudumiwa katika kuwapa sauti watu wenye ulemavu.

 

Mkutano huu uliwapatia fursa viongozi wa kijamii na serikali kufikisha ujumbe wao haswa watu wenye ulemavu waliohudhuria waliweza kutambua vema ni kipi kinaendelea juu yao kuhusiana na hali halisi ya maisha yao.Kupitia utafiti huu na mkutano kwa ujumla wadau kadhaa waliweka ahadi mbele ya wadau pia mioyoni mwao kuwasaidia watu wenye ulemavu.

 

Hakika ili kuwa siku ya mwanga mpya kwa watu wenye ulemavu kukutana kwa pamoja na kujadili mambo yanayowagusa moja kwa moja wakiwa na jamii tofautitofauti maana walikuwepo wadau toka ndani na nje ya mkoa wa Kagera ambao walitoa  mwamko mpya katika maisha ya watu wenye ulemavu na jamii kwa ujumla.

 

1.1  Mahudhurio

Namshukuru   Mungu kuwa lengo lilitimia la kutoa taarifa ya hali halisi ya watu wenye ulemavu hapa Karagwe kwani viongozi wa kada mbalimbali waliweza kuhudhuria mkutano huu.Jumla ya wadau 85 walihudhuria mkutano huu ambapo viongozi wa madhehebu mbalimbali walihudhuriaviongozi wa kada mbalimbali wa kijamii na serikali pia nao walijumuika katika mkutano huu na kuleta maana halisi ya mkutano wadau.

Uwepo wa meneja msaidizi wa shirika la kuhudumia watu wenye nchini la CCBRT ambalo lina makao  yake makuu Msasani jijini Dar es salaam ilikuwa ni mwanga mpya kwa watu wenye ulemavu ,kuwepo wa mwakilishi kutoka IZAAS MEDICAL CENTRE kutoka Bukoba,mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya wenye ulemavu mkoa wa KAGERA na katibu wake nao uliwapa fursa wadau kujua nini maana halisi ya ulemavu pia kujua lugha ambazo hazileti unyanyaapaa kwa watu wenye ulemavu hapa Karagwe.Mgeni rasmi ambaye alikuwa katibu Tawala wa wilaya ya Karagwe akimwakilisha mkuu wa wilaya COL  Mstaafu Suleiman Issa Njiku,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe Kasunju  Runyogote pia kulileta maana halisi ya mkutano wa wadau.

 

Vyombo vya habari navyo vilikuwa bega kwa bega kuhakikisha vinatoa sapoti  muhimu katika kuhamasisha kwa undani zaidi ili jamii iweze kushiriki kikamilifu kupigania haki na maslahi ya watu wenye ulemavu zinatekelezeka..Wana habari  walioweza kufika katika mkutano huu ni kutoka Sengerema FM-Mwanza,  Kasibante  Fm-Bukoba,Vision FM-Bukoba,Karagwe  FM ,Fadeco   Fm na waandishi wa Magazeti ,Blogs na taasisi ambzo zinashiriki kutoa elimu ya habari hapa nchini.Mwakili wa kutoka shirika la utangazaji la  Uingereza  BBC, Tony aliyezungumzia umuhimu wa vyombo vya habari katika kuisaidia jamii katika kufikia malengo yake kikamilifu.

 

Kuwa na idadi hiyo ya wageni ilileta na kuvuta hisia za wazi kwa watu waliohudhuria mkutano huu kiasi kwamba kuuliza mliwezaje kufanya kazi hii yenye kuhitaji uvumilivu.

Haya ndio maudhulio ambao waliweza kushiriki nasi katika uwasilishaji wa ripoti yetu ya utafiti.

 

1.2  GHARAMA ZA KUENDESHA  MKUTANO.

Haikuwa kazi rahisi kuandaa na kuendesha mkutano huu maana  ilihitaji gharama  za mkutao huu.Mkutano huu ulikuwa umegawanyika katika makundi mengi tu kwani kuna watu wenye ulemavu kusafirishwa kulazwa ,kuhudumiwa kila aina ya huduma zote muhimu za kibinadamu.

 

Katika mkutano  huu ambao ulirushwa moja kwa moja na redio Fadeco uliweza kuteka hisia za wanajamii na wasikilizaji wote ambao walikuwa wakifuatilia mkutano huu moja kwa moja kwa maana redio  Fadeco inasikika wilaya zote za mkoa huu wa Kagera na maeneo jirani ya nchi ya Uganda.

 

Jamii ya wilaya ya Karagwe na mkoa wa Kagera kwa ujumla ilikuwa haijui baadhi ya aina za ulemavu lakini baada ya mkutano huu imeweza kubaini ni nini maana ya ulemavu na aina za ulemavu,pia kujua ni lugha ipi itumike ili kukomesha tabia ya unyanyapaaji wa watu wenye ulemavu. Lakini pia jamii imekuwa na uwezo wa kubaini watu wenye ulemavu kwa sasa na kwa asilimia nyingi wanajua nini faida ya kuwafichua watu wenye ulemavu maana mwanzo hawakujua umuhimu huo.

 

Watu wenye ulemavu  waliokuwa na wao wakijinyanyapaa wameweza kufahamu wanalopaswa kulitenda hivi sasa hawajifichi tena maana kupitia idadi kubwa ya watu wenye tatizo la FISTULA wamejitokeza kwa wingi baada ya mkutano huu ambapo shirika la CCBRT kutangaza rasmi kuwa linasafirisha wenye tatizo la Fistula na mdomo wazi kuwa matibabu ni bure.

 

1.3  MCHANGO WA VIONGOZI WA DINI,SERIKALI NA TAASISI.

 

Kupitia mkutano huu wadau wa maendeleo ngazi mbalimbali waliweza kutoa ahadi zenye kuleta matumaini kwa watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kupunguza hali duni za watu wenye ulemavu ili waweze kukabiliana na changamoto walizonazo.

 

Mkurugenzi wa shirika la WOMEDA  Juma Masisi ambaye ni mwanasheria kitaaluma aliweza kusema atashirikiana bega kwa bega ili kuwasaidia watu wenye ulemavu ktk utetezi wa haki zao.,Kanisa la KKKT kupitia idara ya Udiyakonia ambayo hushughulika na watu wenye mahitaji maalumu katika jamii kuhaidi kuwa itaweza kushirikiana kwa karibu na watu wenye ulemavu.Kanisa Katoliki jimbo la Kayanga kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya kujenga shule ya watoto wenye mahitaji maalumu katika eneo la Chabalisha ili kuwapa fursa ya kupata haki yaoya msingiya elimu.

 

Serikali kupitia kwa hotuba ya mgeni rasmi pia mwenyekiti wa halmashauri ndugu Kasunju Runyogote alibainisha hatua ambazo zimechukuliwa na halmashauri katika kuwahudumia watu wenye ulemavu ikiwa ni pomoja na kutenga sh 95 milion katika mwaka wa bajeti wa 2012/2013 kukamilisha ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu eneo la Chabalisha, kuwatengea sh million 5 kwa ajili ya kuendesha miradi midogo midogo kwa watu wenye ulemavu,imewapatia ofisi ambazo ziko katika jengo la Angaza  Kayanga,sh milioni 2 zimetolewa kwa ajili ya kuendeleza karakana ya watu wenye ulemavu  pia kuwasomesha walimu wa elimu maalumu ili waweze kufundisha katika shule hiyo.

 

2.0 MAFANIKIO YALIYOTOKANA NA MKUTANO  HUU

 

Mafanikio ambayo yametokana na mkutano huu ni ya kujivunia hata kama si ya kujiridhisha kwa kiasi kilichokuwa kinahitajika lakini yafuatayo ni moja ya ishara ya mafanikio makubwa ya mkutano huu hii ni pamoja na

 

i)Jamii kutambua kuwepo na idadi kubwa ya watu wenye ulemavu na aina mbalimbali za ulemavu hapa Karagwe

 

ii) Kufahamu jukumu la viongozi ,wadau na jamii katika kuwahudumia watu wenye ulemavu katika wilaya ya Karagwe na mkoa kwa ujumla

 

iii)Viongozi ,wadau, na jamii kutoa tamko la kujifunga la kutekeleza jukumu la kuwahudumia wadu wenye ulemavu na makundi yenye mahitaji muhimu.

 

iv)Watu wenye ulemavu kupata fursa ya kukutana kwa pamoja kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo na jamii na kuionesha kuwa na wao wana uwezo stahiki ktk maendeleo kwa kutumia fursa zilizopo kwa ukamilifu.

 

V)Kuwepo mwanzo mpya wa matibabu kwa watu walikuwa wamekwisha kata tama ya kupona watu wenye matatizo ya ugonjwa wa FISTULA  kuweza kupata matibabu bure.

vi)Kuondoa unyanyapaa miongoni mwa jamii lakini na kwa watu wenye ulemavu wenyewe maana walikuwa wanashindwa kujitokeza

 

vii)Kuondoa imani potofu ya kuamini kuwa ulemavu mwingine ni wa kurogwa au kuwa ulemavu ni laana lakini hiyo mitizamo imeweza kuanza kutoweka baada ya mkutano huo.

 

Viii) Kuwepo idadi kubwa ya wanawake wenye tatizo la Fistula kujitokeza kwa wingi kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wa Kagera baada ya Radeo  FADECO kurusha mkutano huu,Kwani mpaka sasa wagonjwa wapatao 16 wameisha safirishwa kwenda kutibiwa jijini Dar es salaam

 

ix) Serikali ya halmashauri kuamua kutenga bajeti kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuwawezesha  kuanzisha miradi midogo midogo

 

x)Kuwepo  jitihada za kuunda vikundi kwa ajili ya kuwawezesha kuwa na vikundi imara.

 

Haya ni moja ya mafanikio ya mkutano huu lakini yapo mengi yaliyotokana   na mkutano huu pia kuwepo na mwamusho mpya wa kuwa na mtandao wa watu wenye ulemavu.

2.1 HITIMISHO

Nahitimisha kwa kuwaasa wadau wote wa maendeleo wazawa tusisubilie misaada ya wahisani bali tunaweza kutatua  matatizo yetu wenyewe bila ya kumtegemea mtu au wahisani ni jukumu moja linalohitajika ni kuwa na moyo wa kujituma na wa kizalendo zaidi katika kuwahudumiawatu wenye mahitaji maalumu.

KUMBE NIMEAMINI INAWEZEKANA KUWA NA MOYO WA KIZALENDO.

AHSANTENI

Advertisements
Posted in News from Karagwe - Tanzania | Leave a comment

Vyanzo vya maji moto ni njia mbadala wa kutengeneza nishati ya umeme

Habari hii ni kutoka NAIVASHA, KENYA, 27.4.2012

Wakati nchi iko katika mikakati ya kuanzisha vyanzo mbadala vya umeme kwa ajili ya kupata nishati ya kuchochea ukuuaji wa viwanda na kuboresha maisha ya wananchi, imebaika kuwa, vyanzo ya maji moto kama vile cha Mtagata katika kata ya Kamuli, vyaweza kuwa moja wapo ya kuzalisha umeme.

Maps showing the Olikario Geo-thermal plantHayo yamebainiwa na Mkrugenzi wa radio FADECO Joseph Sekiku, alipotembelea mradi wa kufufua umeme kutokana na mvuke utokanao na maji moto yanayobubujika kutoka ardhini ulioko katika wilaya ya Naivasha nchini kenya. Hapo jana, Bw. Sekiku ametembelea mradi huu ujulikanao kama OLIKARIA GEO-THERMAL PLANT ulioko nje kidogo ya mji wa Naivasha.

Mradi huu uliozinduliwa mwaka 2004 na rais Mwai Kibaki wa kenya, unao uwezo wa kuzalisha mega watts 105 za umeme kutokana na nguvu za mvuke kutoka ardhini. Mradi huu umeelezwa kuwa wa kwanza barani Afrika, na kuwepo kwa mradi huu, kumeweza kupunguza shida za umeme hasa kukatikakatika mara kwa mara na kutokuwa na umeme wa kuendesha shughuri za maendeleo.

Akizungumza na mtaalamu katika mradi huu, Bw. Kamau ambaye amekuwepo kuzungumza kuhusu mradi huu, amesema kuwa, hadi sasa, mradi huu umeweza kutoshereza mahitaji ya umeme kwa nchi wa kenya kwa asilimia 65% na kwamba, ifikapo mwaka 2015, Kenya itakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa kujitoshereza na mwingine kuwauzia nchi jirani hasa Somalia na Ethiopia.kibao kinachoonyesha eneo la mradi wa geo-thermal, Olikario

Tekinolojia ya kufufua umeme kutokana na mvuke:

Joto kutoka ardhi, pia joto ardhi (Kiing.geothermal energy” kutoka Kigiriki geo =ardhi na thermos = joto) ni chanzo cha nishati kinachotumia joto lililopo katika ganda la dunia. Joto hili latokana na mchakato wa kinyuklia ndani ya tufe la dunia na kiasi kidogo kutoka joto la jua linalopokelewa kwenye uso wa dunia.

Tangu siku za kale watu walijua mahali kadhaa ambako maji ya moto yanatoka kwenye ardhi kama chemchemi. Kama chemchemi hizi za moto zilkuwa karibu na makazi ya watu zilitumiwa kwa kuogelea au hata kupasha moto nyumba kwenye mazigira baridi.

Lakini siku za nyuma watu waligundua mbinu kulitumia joto kutoka ardhi kwa kuzalisha umeme.[1] Mwaka 2007 takriban gigawati 10 za umeme zilipatikana kutokana na matumizi ya jotoa kutoka ardhini ambazo zilikuwa 0.3% ya mahitaji yote ya umeme duniani lakini katika nchi kadhaa kama Iceland au Kenya asilimia ilikuwa kubwa zaidi.

Katika mazingira ya volkeno joto kutoka ganda linafikia uso wa dunia na hapa ni rahisi kutumia mvuke unaotoka au akiba za maji moto zilizopo mita chache chin ya uso wa ardhi kuendesha rafadha za kutengeneza umeme. Nafasi hii iko pia katika sehemu za Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki ambako hadi sasa kuna vituo 3 vya joto ardhi katika Olkaria. [2].

Katika mazingira ya kawaida pasipo na volkeno au njia za magma zinazokaribia uso wa dunia kuna uwezekano kupeleka mabomba ardhini na kupitisha kiowevo kwa pampu katika mabomba haya chini ya ardhi. Tofauti ya joto kati ya kina ambako mabomba yanafikia na uso wa dunia hutumiwa kwa kupashaia nyumba joto au baridi.

Kama kiwango cha joto kinachotolewa ardhini hakizidi kiwango kinachozalishwa katika kina ya ardhi nishati inayopatikana hapa ni kama nishati mbadala.

MAPENDEKEZO KWA SERIKALI YA TANZANIA:

Kwa wakati huu serikali ya Tanzania inayo mikakati ya kuanzisha miradi ya kufufua umeme nchini ikiwemo kutumia nguvu za maji (HYDRO ELECTRICITY POWER GENERATION) katika mto Kagera na mito mingine nchini, kutumia mkaa ya mawe, kutumia gesi asilia (NATURAL GAS) na mikakati mingine mingi.

Kwa muda kaadha, Tanzania imekumbwa na uhaba mkubwa wa umeme kutokana na upungufu mkubwa wa maji katika mito na mabwawa ya kuweka maji ya kuzalisha umeme, na kupanda kwa gharama ya mafuta. Jambo hili limekwamisha maendeleo katika maeneo mengi na limeacha serikali ikiumia baada ya kulazimika kuanzisha miradi mingine mbadala ambayo imejifanya kutumia pesa nyingi na kubaki na madeni makubwa.

Kama ambavyo inakumbukwa, mgawo wa umeme umekuwa kitu cha kawaidia katika miji mikubwa huku uzalishaji ukishuka kwa asilimia kubwa. Awali, serikali iliingizwa katika matatizo baada ya kuingia katika makubaliano na makampuni kama vile ya Dowans katika kujaribu kutatua changamoto za uhaba wa umeme.

Hali ya umeme wilayani Karagwe:

Wilaya ya Karagwe ni miongoni mwa wilaya chache za nchi na mkoa wa Kagera
ambazo zinafaidika moja kwa moja na umeme unaotoka Uganda kupitia maporomoko
ya mto Nile. Hapa hakuna mgawo wala nini, umeme upo tu saa 24, ukiondoa siku
chache mno za services. Lakini ni wananchi wangapi wanatumia umeme? Umeme
umeingia Karagwe kwa kufuata njia kuu ya Kyaka tokea Bukoba hivyo
unapatikana tu kwenye maeneo ya njia kuu hii.

Sina takwimu sahihi lakini ninaamini umeme unapatikana kwenye maeneo ya njia
kuu ya Bukoba Karagwe hususani kwenye taasisi za serikali kama gereza la
Kitengule, Kikurura Ranchi, Kihanga, Kayanga yaliko makao makuu ya wilaya,
Omurushaka mji wa biashara na maeneo jirani na miji hii, basi! Hii ni kama
asilimia 1.5 ya wilaya ya karagwe.

Njia ya kuelekea Rwambaizi, umeme unaishia Ndama na katika njia ya kuelekea Nkwenda, umeme unaishia Ihanda. Njia ya kuelekea Bushangaro umeme unaishia kijiji cha Nyakahanga wakati njia ya kuelekea Nyaishozi kwa wakati huu pia umeme unaishia katika kijiji cha Nyakahanga.

Nimatumaini yangu kuwa mpango wa REA utawawezesha wakazi wengi wilayani karagwe kuonja utaamu wa umeme kwani tayari nguzo za umeme zimeisha tandazwa hadi Ihembe, ambapo matumaini kwa wakazi wa Bisheshe, Nyakayanja, Nyaishozi hadi Ihembe tayari wameanza kufanya wiring ya nyumba zao wakisubiri umeme kuwasili. Kwa wakazi wa maeneo mengine wilayani Karagwe, yawapasa kuwa na subira.

Mpango wa kufufua umeme mbadala kwa maeneo baadhi wilayani Karagwe:

Katika mto wa Kagera, upo mpango wa kufufua umeme katika eneo la Rusmo wilayani Ngara. Umeme huu utawezesha wananchi wa wilaya hususani ya Ngara, ambao hadi sasa umeme wao unatokana na genereta zinazotumia mafuta, kupata umeme wa kuaminika. Pia upo mpango wa kufufua mradi wa kutengeneza umeme wa Kikagati (karibu na Murongo) ambao unatarajia kuwanufaisha wakazi wa wilaya mpya ya Kyerwa.small hot water spring trapped for hot water domestic use

Na katika mantiki hii, eneo la mtagata katika kata ya kamuli, nalo laweza kujipatia umeme wa geo-thermal kutokana na chanzo cha maji moto katika eneo hilo.

Posted in News from Karagwe - Tanzania, Uncategorized | Leave a comment

Fadeco Community Radio – Karagwe Tanzania

A community Radio that was started in 2007,broadcasting in Kiswahili language in Tanzania with an estimated audience of above 5, million listeners , spread across North west part of Tanzania with an extended coverage in neighbouring countries, Uganda,Rwanda and Burundi.

 Vision of radio FADECO        

 A happy and prosperous community which is knowledgeable about current affairs and news around themselves at all times and is actively involved in day to day development undertakings.

 Mission of radio FADECO

 To stimulate rural development by facilitating access to and dissemination of information, learning resources and communication technologies in Karagwe district; and to become the leading community radio contributing to the economic and social development of the Karagwe Communities and the nation at large.

 Objectives of Radio FADECO

         To Provide, disseminate and exchange development information to the people in Karagwe district so that they can actively participate in national development and to provide affordable communication and information services to meet the socioeconomic and cultural needs of everyone in Karagwe District.”

       Help the rural communities to uphold and preserve their cultures (indigenous knowledge, practices and traditions) and help them live harmoniously live with each other and the environment. 

    To support the work of evangelization through broadcasting catechetical teaching and religious programs (including mass on Sunday and other holy days and festivities) and Christian doctrine (music, liturgy) so that, the church can reach out to more people easily and quickly.

Posted in Uncategorized | Leave a comment

Hello world!

Welcome to WordPress.com! This is your very first post. Click the Edit link to modify or delete it, or start a new post. If you like, use this post to tell readers why you started this blog and what you plan to do with it.

Happy blogging!

Posted in Uncategorized | 1 Comment