MACHACKOS, Kenya
Utabiri wa hali ya hewa ni muhimu sana katika kumusaidia mkulima kuweza kufanya mipangilio mizuri ya shughuri zake za uzalishaji.
Hayo yemebainishwa katika mkutano ambao umefanyika leo katika wilaya ya Machakos nchini Kenya, katika kituo cha utafiti cha kilimo kilichopo Katumani. Kituo hiki cha Katumani ni moja ya vituo 23 nchini Kenya vinavyoendeshwa na kituo cha utafiti cha kilimo cha Kenya Agricultural Research Institute (KARI). Pamoja na mambo mengine kituo cha Katumini kimejikita katika kuwasaidia wakulima kukabiliana na chnagamot za mabadiliko ya tabia nchi (climate change) kwani eneo hili la Machakos ni moja wapo ya maeneo yaliyopo katika nyanda kame.
Mkutano wa leo umehudhuriwa na waandishi wa habari kutoka nchi za kenya, Tanzania, Burundi pamoja na Uingereza. Mkutano huu umefuatiwa ziara katika kikundi cha wakulima wanaotumia taarifa za utabiri wa hali ya hewa zitolewazo na kituo hiki cha Katumani KARI.