FADECO YAENDESHA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NA WATANGAZI JINSI YA KURIPOTI MASUALA YAHUSUYO WATU WENYE ULEMAVU KUANZIA 12-14 April 2012, Kayanga, Karagwe. na Juhudi Felix

Waandishi wa habari wameombwa kutumia vipaji vyao na elimu waliyo nayo, ili kutoa fursa kwa makundi ya watu wasio kuwa na sauti, ili waweze kusikilizwa.

Hayo yamesemwa na Mkrugenzi wa radio FADECO katika mafunzo ya siku 3 kwa waandishi wa habari na watangazaji wa radio, kuhusu mbinu za kuripoti masuala yanahusu jamii wakiwemo watu wenye ulemavu. Mafunzo haya yamewahusisha waandishi wa habari na watangazaji kutoka Radio 5 zikiwemo: Radio FADECO, Radio Vision FM, radio Kasibante, radio Karagwe pamoja na Radio Sengerema FM.

Mafunzo haya yamewezeshwa na Bw. Juhudi Felix ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha maendeleo ya jamii cha Musoma kwa kushirikiana na Bw. Kaspar kutoka shirika la CCBRT la jijini Dar es esalam, Bw. Valerian Rugemalira ambaye ni Mkrugenzi na mwanzilishi wa radio VISION FM ya Bukoba, Bw. Aggrey Mashanda kutoka shirika la kanisa la Anglikana na KCBR pamoja na Bw. Juma Masisi kutoka shirika ka kutetea haki za kisheria za wanawake WOMEDA.

Lengo la kuwa na semina kwa waandishi wa habari ulikuwa ni mwendelezo wa kuwapa sauti watu wenye ulemavu ilikuweza kukabiliana na changamoto ambazo zinazowakabili watu wenye ulemavu ili kuangalia ni kwa namna gani waandishi wanaweza kuchochea jamii ili iweze kuungana kwa pamoja kuleta usawa katika maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Katika mafunzo kwa waandishi wa habari ambayo yalikutanisha waandishi kutoka vyombo vya habari mbalimbali vya ndani ya mkoa wa Kagera na nje ya mkoa ikiwemo Radio Sengerema FM –Mwanza,  jumla ya waandishi wapatao 25 walipatiwa mafunzo ya jinsi gani ya kuripoti habari kwa usahihi juu ya watu wenye ulemavu na makundi mengine yenye mahitaji maalumu.

Mafunzo kwa waandishi wa habari yalijikita katika  nyanja za-

i)Kuandaa vipindi vinavyogusa jamii juu ya watu wenye ulemavu

ii) Matumizi sahihi ya lugha katika kuripoti habari ili kuepuka unyanyapaaji

iii) Kuripoti habari zinazowagusa watu wenye mahitaji maalumu

iv)Kuwa na ufahamu sahihi aina za ulemavu na maana yake

v) Kuwabaini watu wenye ulemavu katika maeneo wakofanyia kazi zao

vi)Mafanikio ya mafunzo haya ni kuwa na  ufahamu juu ya watu wenye ulemavu

Katika mafunzo haya katika siku ya mwishi wa mafunzo, waandishi wa habari waliweza kupata fursa ya kutembelea kiliniki ya wataalamu kutoka hospitali ya Kagondo waliokuwa katika eneo la ofisi ya shirika la KCBR ambapo wanahusika na kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu hapo waliweza kujifunza mengi.

Mbali na kuwa mafunzo haya yalitolewa, pia changamoto kwa upande wa pili haziwezi kukosa maana  tumekumbana na hizi ni kwa vipi mpango utatekelezwa ,viongozi kutokuwa tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa habari,watu wenye ulemavu kujinyanyapaa wenyewe na kutokuwa tayari kutoa ushirikiano.

KUANDAA VIPINDI VINAVYOGUSA JAMII

Katika mafunzo haya waandishi walifundishwa kuandaa vipindi vyenye kugusa hisia za wanajamii katika kutetea watu wenye ulemavu ili kuondoa hali ya unyanyapaa ambao upo katika jamii inayowazungunguka.Katika mada hii njia za ufundishi.

Waandishi waliohudhuria semina kwa ajili ya kuandika kwea usahihi habari zinazogusa makundi maalumu katika jamii waliweza kupata ujuzi na mbinu sahihi ya kuripoti na kuandaa vipindi hivyo.

MATUMIZI SAHIHI YA LUGHA KATIKA KURIPOTI HABARI

 Katika mafunzo kwa waandishi wa habari yalitolewa yalikuwa maalumu kwa ajili ya kuwawezesha waandishi wa habari kuwa na upeo sahihi kuhusiana na lugha mbadala ya kutumia ili kuepuka kutumia lugha ambayo inaleta unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu na makundi mengine maalumu.

Kuwa na mbinu mbadala za kuzungumzia ili kuweza kuwabaini watu wenye ulemavu na kuwezesha jamii kutambua jukumu ililonalo katika kuwahudumia watu wenye ulemavu na watu wengine.

Katika mafunzo haya ambayo yalikuwa ya nadharia na kwa vitendo yaliwajenga haswa kwa kugusa hisia zao jambo lililopelekea baadhi ya waandishi kuweka nadhiri ya kutimiza majukumu yao katika kuwahudumia watu wenye ulemavu kikamilifu.

MAFANIKIO YA MAFUNZO YA WAANDISHI WA HABARI.

Mafanikio yaliyotokana na mafunzo haya ni kuwepo mabadiliko katika kuripoti habari za watu wenye ulemavu kutoka sehemu mbalimbali za mkoa huu wa Kagera na hata nje ya mkoa wa Kagera.Mfano mwandishi Thomas  Bahati wa Bukoba vijijini aliweza kuwabaini watu wenye tatizo la Fistula na kuweza kuwasindikiza mpaka Bukoba mjini na wamesafirishwa mpaka jijini Dar es salaam kutibiwa.

Pia Nyerere Stephano aliweza kumbaini mama ambaye ni mlemavu wa viungo ambaye yuko kata ya Igurwa hawezi kunyanyuka mahali alipo hivyo na kumwezesha kupaza sauti yake.

Kuwepo waandishi mbalimbali kutumia njia nyinginezo kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusiana na watu wenye ulemavu ili watambue kuwa hili ni tatizo katika jamii yetu.Waandishi hao ni Matrida Blasio ambaye ni mwandishi na mtangazaji wa VISION FM iliyopo Bukoba ambaye ameweza kuhamasisha waandishi wenzake kuanza kuripoti habari za watu wenye ulemavu,Nicolaus  Mac  Ngaiza mtangazaji wa KASIBANTE  FM ya Bukoba kuanza kuripoti  kwa kina habari za watu wenye ulemavu pia ameweza kutumia blog yake ya www.kandayaziwa.blogspot.com kuchapisha baadhi ya taarifa za mkutano uliofanyika pia mafunzo ya waandishi wa habari,Mwandishi Emmanuel Julius kutumia blog yake ya www.emmanuel.blogspo.com kuchapisha habari za watu wenye ulemavu,Jacksoni Julius naye kutumia blog yake ya www.jacksonmpare.blogspo.com kutangaza habari za watu wenye ulemavu vilevile kupitia blog ya www.juhudkaragwe.blogspot.com unapata habari za watu wenye ulemavu kwa kina zaidi pia waandishi wa redio SengeremaSweetbetha Mganga na Donasian Kamambi ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Sauti ya Watu Wenye Ulemavu  katika Redio Sengerema –Mwanza kutoa shukruni kwani  ameweza kuwa na mwanzo mpya wa mabadiliko katika kuandaa vipindi vya kuigusa jamii baada ya kuhudhuria mafunzo haya.Donasiani Kamambi pia ndiye mwenyekiti wa shirikishio la SHIVIWATA wilaya ya SENGEREMA-MWANZA.

HITIMISHO

Huo ndio ulikuwa ndio Mwanzo mpya wa safari ya waandishi katika kuihabari jamii juu ya watu wenye ulemavu kujua jukumu lao na nini changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu kushiriki kikamilivu katika kutumia njia mbadala za kuondoa unyanyapaa wa aina yoyote ile na mitazamo hasia miongoni mwa jamii.

Jamii inaweza kubadili mtazamo hasia kwenda chanya na kushiriki kikamilifu katika kupinga unyanyapaa wa aina yoyote ile kwa mtu yoyote yule endapo waandishi wa habari na vyombo wanavyovitumikia kuwa na nia ya dhati na maono ya kuitumikia jamii haswa kwani jukumu la mwandishi wa habari na chombo cha habari ni kuitumikia jamii.

Tukiongozwa na utume au (Mission)tukiitumia kikamilifu tatizo la watu wenye ulemavu litakuwa ni simuli na halitakuwa tena tatizo kama ilivyo sasa.

Mwisho nikuombee wewe binafsi Mungu akuzidishie Muda wa kuishi ili uweze kuwasaidia watu wengine wenye kuhitaji msaada kwani kuna watu wamesahauliwa isingekuwa ni wewe ni nani leo hii angelikuwa anazungumza habari ya tatizo la fistula kwa kina hapa Karagwe?

KUMBE TUKIACHA KUCHANGIA HARUSI NA MENGINE AMBAYO HAYANA MANUFAA KAMA BITHDAY  PARTY,KICHEN PARTY Tutaondokana na matatizo haya ikiwemo kutumia raslimali vizuri inawezekana.

About fadeco

Media expert from Tanzania.
This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s